max

kamwini

printer

Thursday, November 8, 2012

KASEJA AIBUKA KAMA MTAZAMAJI MAZOEZINI SIMBA


Kaseja akiomba dua katika moja ya mechi za timu hiyo


NAHODHA wa Simba, Juma Kaseja kwa siku ya tatu mfululizo jana ameendelea na mgomo wake wa mazoezi ya timu yake inayojiandaa na mchezo wa mwisho wa mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, utakaopigwa kesho Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, huku kukiwa kuna habari ameamua kuachana na timu hiyo.
Lakini tofauti na siku mbili za awali, Kaseja jana alifika kwenye Uwanja wa Kinesi, ila mtazamaji kama watazamaji wengine.
Hakufanya mazoezi, ingawa alipoulizwa alisema yeye bado bado mchezaji wa Simba na ana mkataba na timu hiyo.
Mwanzoni mwa wiki ilielezwa kwamba Kaseja amewaaga wachezaji wenzake na kuwaambia yeye na klabu hiyo basi.
Hatua hiyo ilifuatia Kaseja kutukanwa na kutishiwa maisha na mashabiki wa Simba baada ya mechi dhidi ya Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro wakimtuhumu kufungwa mabao ya kizembe.
Lakini tayari uongozi wa Simba umelaani vikali vurugu na vitisho alivyotolewa kipa wao huyo namba moja,  na kusema wanafikiria kuwachukulia hatua kali watu waliomfanyia hivyo Nahodha wao huyo. 

No comments:

Post a Comment