max

kamwini

printer

Thursday, November 8, 2012

KASEJA AIBUKA KAMA MTAZAMAJI MAZOEZINI SIMBA


Kaseja akiomba dua katika moja ya mechi za timu hiyo


NAHODHA wa Simba, Juma Kaseja kwa siku ya tatu mfululizo jana ameendelea na mgomo wake wa mazoezi ya timu yake inayojiandaa na mchezo wa mwisho wa mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, utakaopigwa kesho Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, huku kukiwa kuna habari ameamua kuachana na timu hiyo.
Lakini tofauti na siku mbili za awali, Kaseja jana alifika kwenye Uwanja wa Kinesi, ila mtazamaji kama watazamaji wengine.
Hakufanya mazoezi, ingawa alipoulizwa alisema yeye bado bado mchezaji wa Simba na ana mkataba na timu hiyo.
Mwanzoni mwa wiki ilielezwa kwamba Kaseja amewaaga wachezaji wenzake na kuwaambia yeye na klabu hiyo basi.
Hatua hiyo ilifuatia Kaseja kutukanwa na kutishiwa maisha na mashabiki wa Simba baada ya mechi dhidi ya Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro wakimtuhumu kufungwa mabao ya kizembe.
Lakini tayari uongozi wa Simba umelaani vikali vurugu na vitisho alivyotolewa kipa wao huyo namba moja,  na kusema wanafikiria kuwachukulia hatua kali watu waliomfanyia hivyo Nahodha wao huyo. 

MILAN KUMNYOFOA BACARY SAGNA ARSENAL



Gossip logo
8 November 2012Last updated at 23:44 GMT

INTER MILAN KUMNYOFOA BACARY SAGNA ARSENAL

Inter Milan ipo tayari kumnasa beki wa kulia wa Arsenal, Bacary Sagna, mwenye umri wa miaka 29, mwishoni mwa msimu.
Manchester United wampiga kasi katika jitihada zao za kumsajili kiungo Mkenya mwenye umri wa miaka 21, anayechezea Celtic, Victor Wanyama, ambaye alifunga bao katika ushindi wa 2-1 wa timu yake dhidi ya Barcelona juzi.
Charlie Austin
Nyota wa Burnley, Charlie Austin anayetakiwa na Arsenal
Arsenal, Chelsea na Manchester City zimeripotiwa kutoa ofa kwa ajili ya beki wa PSV Eindhoven, Riechedly Bazoer, mwenye umri wa miaka 16.
Beki wa pembeni wa Kibrazil, Wallace, mwenye umri wa miaka 18, yupo mbioni kusaini Chelsea, kwa mujibu wa klabu yake ya sasa, Fluminense.
Habari kamili: Press Association
Arsenal imeungana na orodha ya klabu zinazomfuatilia mshambuliaji wa Burnley mwenye umri wa miaka 23, Charlie Austin.
The Gunners pia wako wanamtaka beki wa kushoto wa PSV na Uholanzi, Jetro Willems, mwenye umri wa miaka 18.
Manchester City inataka kumsajili kinda wa Chelsea mwenye umri wa miaka 16, Conor Hunte.
Chelsea imeripotiwa kutaka kumsajili mshambuliaji wa Vitesse Arnhem, Wilfried Bony, mwenye umri wa miaka 23, ambaye amekuwa akiitwa 'new Didier Drogba'.